Wednesday, December 12, 2012

BAADA YA KUPIGWA MKWARA RPC KINONDONI(REGION POLICE CAMMANDER)AFUTA MKUTANO WA CHADEMA


Katibu Mwenezi wa CCM Nape Nnauye 

KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Charles Kenyela ameuvunja mkutano wa Chadema uliokuwa ufanyike juzi katika Viwanja vya Sigara vilivyopo Sinza ‘B’ Dar es Salaam baada ya viongozi wa CCM wa tawi la eneo hilo kupinga wakisema ukifanyika utasababisha uvunjifu wa amani.
Akizungumza kabla ya mkutano huo uliokuwa umeandaliwa na Chadema Mkoa wa Dar es Salaam, Diwani wa Kata ya Sinza kwa tiketi ya chama hicho, Renatus Pamba alisema walifuata taratibu zote ikiwamo kibali cha polisi.
Kamanda Charles Kenyela alisema juzi kuwa aliuvunja mkutano huo kwa sababu za kiusalama licha ya Chadema kufuata taratibu zote na kuruhusiwa awali.
Alisema kufutwa huko kulitokana na mvutano baina ya chama hicho na wafuasi wanaosadikiwa kuwa ni wa CCM ambao walidai kuwa uwanja huo ni wao.
Hata hivyo, Diwani Pamba alisema eneo hilo ni la wazi na CCM walilivamia kwa kuweka kontena na kufungua tawi.
Sakata hilo liliibuka saa tisa alasiri baada ya Katibu wa Chadema Kata ya Sinza, Bayega Masunga kuvamiwa na watu wanaodhaniwa kuwa ni wafuasi wa CCM na kuanza kumpiga alipokuwa akipanga meza na vitu vingine kwa ajili ya kuanza mkutano.
Baada ya kitendo hicho, eneo hilo liligeuka uwanja wa ghasia hadi polisi Kituo cha Urafiki walipofika eneo hilo. Hata baada ya kufika, askari hao walijaribu kutafuta ufumbuzi wa suala hilo bila mafanikio ndipo walipomfahamisha Kenyela.
Baada ya kusikiliza malalamiko ya pande zote mbili, Kenyela alisema Chadema walikuwa na haki ya kufanya mkutano huo.
Hata hivyo uamuzi huo uligomewa na viongozi wa CCM wa eneo hilo na wafuasi wao ambao walimzonga Kenyela na kumtaka azuie mkutano wakisema lolote linaweza kutokea kwa kuwa wanawajua vijana wa eneo hilo.
“Mimi naona mkutano uvunjwe labda ufanyike siku nyingine lakini siyo leo kwani ni lazima vurugu zitatokea,” alisema Mwenyekiti wa CCM Tawi hilo, Abdallah Malipula kauli ambayo ilichukuliwa na wanaChadema kuwa ni kuwatisha polisi.
Baada ya mvutano uliochukua muda mrefu, Kenyela alisema anazuia kufanyika kwa mkutano huo kauli ambayo ilipokewa kwa mshangao na wana Chadema ambao walipiga kelele huku wakiimba “CCM, CCM, CCM.”
Akizungumza baada ya uamuzi huo, Diwani Pamba alisema hajui ni kwa vipi magari yapatayo manne yaliyosheheni askari polisi wakiwa na silaha washindwe kusimamia mkutano huo. Alisema hiyo inaonyesha jinsi gani polisi wanavyochangia migogoro katika jamii.
“Ipo wazi, kibali tunacho lakini leo CCM wanasema Chadema wakifanya mkutano lolote linaweza kutokea, RPC anagwaya na kuvunja mkutano wetu hapo kuna nini tena?”

No comments:

Post a Comment

sikiliza ngoma zinazo kamata kwa sasa

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...