Fredy Azzah
HATUA ya mwanazuoni wa siku nyingi nchini, Profesa Issa Shivji kupinga hukumu ya Mahakama ya Rufani Tanzania iliyomrejeshea ubunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema imemtia matatani na baadhi ya watu wanasema gwiji huyo wa sheria “huenda amenukuliwa vibaya au hajasoma hukumu husika.”
Jana Wakili wa Lema, Tundu Lissu, alimkosoa
Profesa Shivji pamoja na Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika,
Francis Stolla akisema wanasheria hao wamepotoka katika matamshi yao ya
kupinga hukumu ya Mahakama ya Rufani.
Matamshi ya Shivji pia yaliiteka mijadala katika
mitandao ya kijamii ya Jamii Forums, Mabadiliko na Facebook ambako
wachangiaji walikuwa wakivutana huku baadhi yao wakisema wazi kwamba
msomi huyo amekosea huku wengine wakimtetea kwamba yuko sahihi.
Akizungumza na gazeti hili jana kutoka Songea
mkoani Ruvuma, Lissu alipinga vikali hoja zilizotolewa na Profesa Shivji
pamoja na Stolla, akisema kuwa hazina mashiko na zinaweza kutolewa tu
na mtu ambaye hakufuatilia mwenendo wa kesi hiyo.
Juzi Profesa Shivji na Stolla walinukuliwa
wakiikosoa hukumu ya Mahakama ya Rufani, iliyomrejesha bungeni Lema
wakisema hukumu hiyo iliyotolewa na majaji watatu Salum Massati, Bernard
Luanda na kiongozi wao Nathalia Kimaro, inapingana na sheria.
Lissu katika maelezo yake alisema uamuzi wa
mahakama katika kesi ya Lema umejenga upya msingi bora wa matumizi ya
vyombo vya uamuzi, kwani kesi nyingi za kupinga matokeo ya ubunge,
zimekuwa zikifunguliwa na watu ambao wamekuwa wakitumwa na vigogo wa
kisiasa na watu wenye fedha.
Akizungumza na Mwananchi, Lissu alisema hoja hizo
hazina mashiko na kuwa ile iliyotolewa na Profesa Shivji inatokana na
msomi huyo kuzungumza kitaalamu bila kuangalia mazingira halisi ya siasa
za Kitanzania.
Lissu alisema mahakama ya rufani haikupiga
marufuku wapiga kura kufungua kesi za kupinga ila iliwataka tu kufanya
hivyo pale haki zao zinapokiukwa.
“Kwanza siyo kweli kwamba mahakama imepiga
marufuku wapiga kura kufungua kesi, ilisema watafanya hivyo pale ambapo
haki zao zimevunjwa, haki zenyewe ni kupiga kura, kura zao kutohesabiwa
ama suala jingine litakalomnyima kupiga kura, hizo ndiyo haki za mpiga
kura,” alisema na kuongeza:
“Sasa mwalimu wangu, Profesa Shivji yeye anatazama
tu kwa jicho la kitaalamu na kusema haki za binadamu zimekiukwa, kwa
muda wanasiasa, matajiri na CCM wamekuwa wakiwatumia wananchi kuwapinga
wabunge wa upinzani.”
Uchambuzi wa Lissu
Alitoa mfano akisema katika uchaguzi wa 1995, Dk Willibrod Slaa alishinda ubunge na watu wanaojiita wananchi walifungua kesi kupinga ushindi huo, mwaka 2000 wakampinga tena na hata 2005.
Uchambuzi wa Lissu
Alitoa mfano akisema katika uchaguzi wa 1995, Dk Willibrod Slaa alishinda ubunge na watu wanaojiita wananchi walifungua kesi kupinga ushindi huo, mwaka 2000 wakampinga tena na hata 2005.
Alisema 1995 Makongoro Nyerere aliposhinda ubunge
katika Jimbo la Arusha Mjini kupitia NCCR- Mageuzi, watu wanaojiita
wananchi walifungua kesi ambayo matokeo yake yalikuwa mbunge huyo
kupoteza kiti chake.
Lissu alisema 2005 aliyekuwa Mbunge wa Tarime,
Marehemu Chacha Wangwe alifunguliwa kesi na watu waliojiita wananchi
ambao mwisho wake walishindwa.
“Hawa wananchi ambao wanafungua kesi zenye mawakili wanaolipwa
mamilioni ya fedha ni watu ambao hata fedha za kununua viatu hawana,
hawa waliokuwa wakimpinga Marehemu Wangwe nikiwa mahakamani niliwauliza
kama wanawajua mawakili waliokuwa wanawatetea, walikuwa hawawajui.
Nikawauliza kama wamewahi kufika Dar es Salaam wakasema hapana, sasa sijui waliwapataje wale mawakili,” alisema na kuongeza:
“Wote hawa wanakuwa ni watu wanaotumiwa. Mwaka
huu kati ya wabunge wote 25 Chadema tulioshinda, 14 tulifunguliwa kesi
na kati ya hizi 12 zimefunguliwa na watu wanaojiita wananchi, hii ni
kutumiwa,” alisema.
Alisema mara baada ya uchaguzi mwaka 2010
aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, aliandika waraka kuwataka
makatibu wa chama hicho kufungua kesi kwa majimbo yote ambayo chama
hicho kiliangushwa jambo alilosema ndilo liliwasukuma kuwatumia
wananchi.
Kuhusu hoja kuwa mahakama hiyo ya rufani
imeingilia kazi ya kutunga sheria badala ya kuzitafsiri na kuwa
imepingana na sheria ya Bunge na Mahakama Kuu katika kesi ya Chediel
Mgonja ya mwaka 1980, Lissu alisema hazina mashiko.
“Hiyo ni hoja ya kipuuzi. Hiyo sheria ya kuwa
mwananchi yeyote ana haki ya kufungua kesi kuwa imetenguliwa na Mahakama
ya Rufani, hata mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa sheria ukimuuliza
atakwambia kuwa, amri ya Mahakama Kuu wala ya Mahakama ya Rufani yenyewe
haiwezi kuizuia mahakama hiyo ya juu kabisa nchini kufanya uamuzi
wake,” alisema.
Akizungumzia hoja ya Stolla kwamba mahakama
iliibua jambo jipya la kuhoji kama wajibu rufani walikuwa wapiga kura
ama la, alisema Rais wake huyo hana hoja, kwani wakili wa walalamikaji
aliibua hoja kama hiyo na alipoulizwa na mmoja wa majaji kuwa “Hata sisi
hatuwezi kulizungumzia suala hili, alishindwa kujibu akawa anajikanyaga
tu,” alisema.
Aliongeza: “Kwenye rufaa ya kwanza mahakama
inaruhusiwa kuibua chochote, sasa hizo ni hoja zinazotolewa na watu
ambao marafiki zao wa CCM wameshindwa sasa wanavaa joho la utaalamu
kutoa hoja kama hizi zisizo na mashiko.”
Shivji na Stolla
Profesa Shivji kwa upande wake alieleza
kushangazwa na maelezo ya Mahakama ya Rufani kuwa mpiga kura hana haki
ya kufungua kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi na kusema hiyo ni sawa
na kutunga sheria mpya na si kutafsiri zilizopo.
“Sheria ya Bunge na Mahakama Kuu katika kesi ya
Mgonja (Chediel ya mwaka 1980), vinampa haki mpiga kura kufungua kesi
mahakamani kupinga matokeo. Sijaona hoja nzito ya Mahakama ya kufuta
haki hiyo ya mpiga kura,” alisema Profesa Shivji.
Kwa upande wake, Stolla alisema: “Nimesikiliza
hata maoni ya wanasheria mbalimbali wakizungumzia kutopendezwa na
tafsiri ya Mahakama ya Rufani kuhusu haki ya mpiga kura ‘ku-challenge’
(kupinga) matokeo ya uchaguzi mahakamani.
Aliongeza: “Katika uamuzi wa kisheria, inaonekana Mahakama
imetunga sheria mpya na wengi tunajiuliza kama siyo, ni sababu gani
nyingine inampa haki mpiga kura kupinga matokeo?”
Stolla alisema Sheria ya Bunge ya Uchaguzi ya
tangu mwaka 1985, ambayo ilifanyiwa marekebisho mwaka 2002, kabla ya
kutungwa upya mwaka 2005, inampa haki mpiga kura kupinga matokeo ya
uchaguzi mahakamani.
Kesi ya Lema
Lema alivuliwa ubunge na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Aprili 5, mwaka huu kutokana na kesi iliyofunguliwa na makada watatu wa CCM, Mussa Mkanga, Happy Kivuyo na Agnes Mollel, wakipinga ushindi wake.
Kesi ya Lema
Lema alivuliwa ubunge na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Aprili 5, mwaka huu kutokana na kesi iliyofunguliwa na makada watatu wa CCM, Mussa Mkanga, Happy Kivuyo na Agnes Mollel, wakipinga ushindi wake.
Walikuwa wakidai kuwa katika kampeni zake alikuwa
akitumia lugha ya matusi, kejeli na ubaguzi wa kijinsia dhidi ya
aliyekuwa mgombea wa wadhifa huo kwa tiketi ya CCM, Dk Batilda Buriani.
Mahakama Kuu katika hukumu yake iliyotolewa na Jaji Gabriel Rwakibarila ilimtia hatiani kwa kutumia lugha ya matusi na kutengua matokeo yaliyompa ushindi.
Hata hivyo, alikata rufaa Mahakama ya Rufani kupitia kwa mawakili wake, Method Kimomogoro na Tundu Lissu ambayo Desemba 21, mwaka huu ilimrejesha tena bungeni baada ya kukubali rufaa yake.
Katika uamuzi wake, Mahakama hiyo ilisema kwa kuwa kisheria hayo ni masilahi ya umma kufikishwa mahakamani chini ya Ibara ya 26 (2) ya Katiba na kwamba mlalamikaji anapaswa kuonyesha haki zake au masilahi ambayo yameingiliwa na athari alizozipata.
Mahakama Kuu katika hukumu yake iliyotolewa na Jaji Gabriel Rwakibarila ilimtia hatiani kwa kutumia lugha ya matusi na kutengua matokeo yaliyompa ushindi.
Hata hivyo, alikata rufaa Mahakama ya Rufani kupitia kwa mawakili wake, Method Kimomogoro na Tundu Lissu ambayo Desemba 21, mwaka huu ilimrejesha tena bungeni baada ya kukubali rufaa yake.
Katika uamuzi wake, Mahakama hiyo ilisema kwa kuwa kisheria hayo ni masilahi ya umma kufikishwa mahakamani chini ya Ibara ya 26 (2) ya Katiba na kwamba mlalamikaji anapaswa kuonyesha haki zake au masilahi ambayo yameingiliwa na athari alizozipata.
No comments:
Post a Comment