Friday, December 14, 2012

HII NDIYO KAULI YASIMBA SPOTS CLUB JUU YA KUVUNJA MKATABA NA MILLOVAN, NA SAKATA LA MRISHO NGASA


.
Hatimae club ya Simba imethibitisha kuvunja mkataba na kocha wake Mserbia Milovan Cicovic ambapo sasa wanatarajia kumtambulisha kocha mpya kutoka Ufaransa.
Namkariri afisa habari wa Simba Ezekiel Kamwaga akisema “huyu kocha ana uzoefu mkubwa sana zaidi ya ukocha wa kufundisha timu kubwa alianzia maisha kwenye Academy, amepitia Academy ya ufaransa ambayo ni maarufu sana na ndiyo iliyotoa kina Thiery Henry wakati huo, mbali na timu kubwa atatutengenezea mfumo mzuri wa kutengeneza timu yetu ya vijana, sasa hivi Tanzania tunashindana na timu mbili za mamilionea”
.
Kwenye line nyingine Kamwaga amesema “atasaidia kukuza viwango vya wachezaji wetu, kama atakua na Simba nzuri manake na timu ya taifa pia itafaidika kwa sababu Simba ndio tegemeo la timu ya taifa ya Tanzania”
Kuhusu ishu nzito ya kumuuza mchezaji Mrisho Ngassa kwenda kucheza Sudan Kamwaga amesema “sisi tumeshakubaliana na Azam kwamba Ngassa akiuzwa basi tutagawana nusu kwa nusu lakini cha msingi Ngassa hawezi kuchezea timu nyingine hapa Tanzania ambayo siyo Simba kwa sababu tuna mkataba nae unaoisha May, Ngassa bado ni mchezaji wetu na tunataraji kwamba mwishoni mwa wiki hii atajiunga kwenye mazoezi na wenzake kwa ajili ya kujiandaa sasa na ligi kuu ya Tanzania na michuano ya kimataifa”
“Wanasema yeye aliongea na hiyo timu ya Sudan na kukubaliana kulipwa dola za kimarekani elfu 70 kwa hiyo Kama atataka kwenda Sudan atakwenda, kama hatokwenda sisi tutamtumia lakini hatuwezi kumpandisha ndege au kumlazimisha, kama atakwenda tutampa ushirikiano kwa asilimia 100 na kama hatotaka kwenda pia tutampa ushirikiano kwa asilimia 100″ – Kamwaga
Kwenye sentensi ya mwisho Kamwaga amesema mlinda mlango namba moja Afrika Mashariki anaetokea Uganda ameshaingia Dar es salaam tayari na anafanyiwa vipimo vya Afya kwenye hospitali moja na kama atafaulu basi atasajiliwa na Simba.

.

No comments:

Post a Comment

sikiliza ngoma zinazo kamata kwa sasa

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...