WIZARA ya Nishati na Madini imesema, Tanzania imelenga uvunaji
wa madini ya Uranium kama nchi nyingi za Afrika zinavyofanya hivi
sasa.Pia, imesema ina Sera ya Madini ya mwaka 2009 na Sheria ya Madini
ya Mwaka 2010 ya kusimamia sekta hiyo.
Taarifa kwa umma iliyotolewa jana na Msemaji wa wizara hiyo, Fadhili Kilewo alikanusha wizara hiyo kutokuwa na sera na sheria za kusimamia uendelezaji madini ya uranium.
Kilewo alisema kumekuwa na maneno kutoka kwa baadhi ya wananchi na wanaharakati kuwa, zoezi la uchimbaji wa uranium lisimamishwe mpaka sera na sheria zitakapotungwa.
“Mengi ya malalamiko hayo yanatokana na uelewa mdogo jinsi serikali ilivyojipanga,” alisema Kiwelo na kuongeza:
“Sera na Sheria hizi zimeweka miongozo ya uendelezaji madini nchini yakiwapo madini ya urani.”
Kiwelo alisema sera na sheria hizo zimehakikisha uendelezaji wa shughuli za madini zinakwenda sambambamba na utunzaji mazingizara.
Alisema uvunaji huo hauna madhara kama inavyoelezwa na wanaharakati.
“Utafutaji wa madini ya urani Tanzania una historia ndefu tofauti na watu wengi wanavyofikiri. Utafutaji huo nchini ulianza mwanzoni mwa mwaka 1970,” alisema.
Alisema utafiti wa kina umekuwa ukiendelea a uliopelekea ugunduzi wa kutosha wa madini hayo
No comments:
Post a Comment