Monday, December 17, 2012

HATIMAYE BODI YA TPA YAKUBALI UWEPO WA UFISADI BANDARINI


Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe  


BODI ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), imekiri wazi kuwa tuhuma za wizi na ubadhirifu zilizoanikwa katika Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) dhidi ya wafanyakazi wa mamlaka hiyo ni za kweli,

Imesema hata hivyo inajipanga ili kuwachukulia hatua za kinidhamu na za kisheria wale wote waliotuhumiwa. Mbali na tuhuma hizo pia kuna madai ya wengi kuhusika katika kutoa zabuni kwa kampuni ambazo hazijasajiliwa, kutoa ajira kwa upendeleo na usimamizi mbovu wa miradi.

Hatua hiyo imekuja wiki tatu tangu bodi hiyo iahidi kuweka hadharani, hatua itakazochukua dhidi ya wafanyakazi hao, baada ya kuipitia ripoti ya CAG.

Hali kadhalika, ripoti ya kamati iliyoundwa Agosti 27 mwaka huu na Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe na ile ya Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA).

Makamu Mwenyekiti wa bodi hiyo, Julius Mamiro alilieleza gazeti hili kwa njia ya mtandao baada ya kuandikiwa maswali na kueleza mikakati ya bodi hiyo huku akisisitiza kwamba ripoti hizo, zinaonyesha kuwa baadhi ya wafanyakazi TPA wanahusika na ubadhirifu.

No comments:

Post a Comment

sikiliza ngoma zinazo kamata kwa sasa

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...