WAKILI wa Serikali Mkuu Timon amedai kuwa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha ilikosea kutengua ubunge wa aliyekuwa Mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema, kwa madai ya kutumia lugha za matusi kwa kuwa Bunge limeruhusu wanasiasa kutukanana kwenye kampeni.
Wakili Vitalis alitoa madai hayo jana, wakati wa
usikilizwaji wa rufaa ya Lema, aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kupitia
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),katika Mahakama ya Rufani
jijini Dar es Salaam.
Wakati wakili huyo wa serikali akitoa madai hayo,
Wakili wa wajibu rufaa, ambao walishinda katika kesi ya msingi, Alute
Mughway, naye alidai kuwa Mahakama Kuu, Arusha ilikosea katika uamuzi
wake, pamoja na mambo mengine, kwa kukataa baadhi ya madai yao.
Lema alivuliwa ubunge April 5, 2012, katika hukumu
iliyotolewa na Jaji Gabriel Rwakibalia, kufuatia kesi iliuyofunguliwa
makada watatu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mussa Mkanga, Happy Kivuyo
na Agnes Mollel, wakipinga ushindi wake katika uchaguzi mkuu wa mwaka
2010.
Lema kupitia kwa Wakili wake Method Kimomogoro
alikata rufaa Mahakama ya Rufani, lakini Novemba 8, 2012 mahakama
ilitupilia mbali rufaa hiyo baada ya kuini kuwepo kwa dosari za
kisheria, kutokana na pingamizi lililowekwa na upande wa wajibu rufaa.
Hata hivyo mahakama hiyo ilimpa nafasi nyingine
ya kukata rufaa tena baada ya kumpa siku 14 kufanya marekebisho ya
dosari hizo za kisheria na kuiwasilisha mahakamani ndani ya muda huo,
amri ambayo aliitekeleaza.
Wakati Lema akikata rufaa kupinga hukumu ya
Mahakama Kuu kumvua ubunge, wajibu rufaa nao walikata rufaa (Cross
Appeal) kupinga uamuzi wa mahakama hiyo, huku wakibainisha hoja nne.
Katika hoja ya kwanza hadi ya tatu walidai kuwa
Jaji alikosea katika hukumu yake kwa kuchanganya vituo vilivyotolewa
ushahidi na mashahidi wanne na hatimaye akakataa ushahidi wapo, pamoja
na tarehe za ratiba ya kampeni ya CCM nay a Chadema.
Hoja ya nne walidai kuwa Jaji alikosea kwa kuamua
kuwa hata kama Lema kwenye kampeni zake alidai kuwa Dk. Buriani ni mkazi
wa Zanzibar hatafaa, wakidai kuwa ukazi si sifa ya kuchaguliwa kuwa
mbunge.
Hatimaye rufaa hizo zilisikilizwa jana na jopo
la Majaji watatu wa Mahakama ya Rufani, lililoundwa na Jaji Salum
Massati, Jaji Bernard Luanda, chini ya uongozi wa Jaji Nathalia Kimaro.
Wakati wa usikilizwaji wa rufaa hiyo, mawakili
wawili ambao ni ndugu, Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lisu na kaka
yake Mghway, walipambana vikali kwa hoja za kisheria.
Lisu, Kada wa Chadema ambaye pia ni Mnadhimu wa
Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, alikuwa akimtetea Lema mrufani (Lema),
akisaidiana na Wakili Method Kimomogolo, huku Mughway akiwatetea wajibu
rufani ambao ni makada wa CCM.
Hata hivyo Wakili Vitalis, aliyemwakilisha Mwanasheria Mkuu wa
Serikali (AG), ambaye pia alikuwa upande wa Lema, alidai kuwa wajibu
rufaa hawakuwa na haki ya kufungua kesi kupinga ushindi wa mrufani
(Lema) kwa kasoro zilizotokea wakati wa kampeni.
Wakili Vitalisi alidai kuwa wajibu rufani hao
hawakuwa wahusika katika katika mchakato huo kampeni na kwamba hata kama
kulikuwa na lugha ya matusi kama walivyodia katika ushahidi wao
mahakama haikuwastahili kumvua ubunge kwa kuwa Bunge liliruhusu matusi
kwenye kampeni.
Akifafanua zaidi Wakili Vitalis alidai kuwa
anayepaswa kufungua kesi mahakamani kwa madai ya lugha ya matusi ni yule
aliyetukana kwa kuwa hayo ni maumivu ya mtu binafsi na kwamba hata
anapokufa, madai yake nayo hufa wala hayawezi kuendelezwa na mtu
mwingine.
“Sasa iweje kwa mtu ambaye yuko hai lakini watu
wengine ndio waje mahakamani kufungua kesi?”, alihoji Wakili wa Serikali
Vitalisi.
Aliongeza kuwa kwa mujibu wa Kifungu cha 108 cha
Sheria ya Uchaguzi Sura ya 313 ya mwaka 2010, matusi si miongoni mwa
mambo ambayo yanaweza kutengua matokeo ya uchaguzi.
Hata hivyo Wakili huyo wa Serikali alidai kuwa
Bunge liliruhusu kutukana na baada ya kufanya marekebisho katika sheria
ya uchaguzi, mwaka 1995 kufuatia hukumu ya kesi kati ya AG na Aman
Waridi Kaburu.
Alidai awali sharia ilikuwa inaruhusu matokeo ya
uchaguzi kutenguliwa kutokana na lugha za matusi, lakini baada ya hukumu
ya kesi ya Kaburu Januari , 1995, mwezi Julai mwaka huo Bunge lilifanya
marekebisho na kuondoa suala la matusi katika mambo yanayoweza kutengua
uchaguzi.
“Hapa Bunge liliifunga mikono mahakama, hakuna
kutengua matokeo ya uchaguzi kwa mambo amabayo hayajatajwa. Kwa uamuzi
huu waliamua kutukanana, kwa hiyo nasi hatuwezi kuwakatalia.”, alidai
Wakili Vitalisi.
Pia alidai kuwa kifungu cha 108 (2) cha Sheria ya
Uchaguzi kinaeleza aina ya za ubaguzi zinazokatazwa ni pamoja na wa
kidini na kikabila na kwamba aina nyingine kama makazi (Uzanzibar,
Ubara) hazijatajwa.
Awali Wakili wa Lema Kimomogoro aliainisha sababu
18 za rufaa hiyo kuwa ni pamoja na Jaji kuamua kuwa Sheria zinazotumika
katika Nchi za Jumuiya ya Madola (hususan Uingereza), hazitumiki katika
kesi za uchaguzi nchini.
Sababu nyingine alidai kuwa ni Jaji kutokujieleza
vyema kama wajibu rufaa waliwajibika katika hati yao ya madai kwa kutaja
maneno dhahiri ya ubaguzi dhidi ya aliyekuwa mgombea wa CCM, Dk Batlida
Burian.
Sababu nyingine alidai kuwa Jaji alikosea kuamua
kuwa mtu yeyote aliyejiandikisha kupiga kura ana haki isiyo na mpaka ya
kufungua kesi kupinga matokeo.
Alidai kuwa hoja yao ni kwamba mtu anakuwa na haki hiyo pale
ambapo haki yake imevunjwa au inaelekea kuvunjwa na si pale
aliyeathirika na ukikwaji wa haki hiyo ni mtu mwingine.
Sababu nyingine alidai kuwa Jaji hakutolea uamuzi
baadhi ya hoja ambazo zilitakiwa kujibiwa na kwamba hakujielekeza vyema
kwenye wajibu wa kuthibitisha madai kwa kueleza kama walalamikaji
walithibitisha madai yao bila kuacha mashaka yoyote.
Sababu nyingine ni kwamba Jaji alitumia ushahidi
wa mdomo bila kungwa mkono na ushahidi mwingine, na kwamba Jaji
alijielekeza vibaya katika kupima ushahidi wa pande zote na badala yake
akaegemea ushahidi wa walalamikaji na mashahidi wao tu.
Pia alidai Jaji alikose kusema kuhusu hoja ya
vitendo vya kijinai na kwamba hakuvitaja hivyo vitendo vilivyofanywa na
mrufani, huku akisisitiza kuwa hukumu hiyo haikukidhi vigezo vya
kisheria.
Hata hivyo akijibu hoja hizo, Wakili Mughwa alidai
kuwa hukumu hiyo imekidhi vigezo vya kuwa hukumu kwa kuwa inaeleza
mambo yote yanayopaswa kuwepo.
Wakili Mughwa alidai kuwa walalamikaji katika kesi
ya msingi kwenye ushahidi wao walieleza maneno yaliyokuwa
yakilalamikiwa huku akidai kuwa mawakili wa utetezi wanaipotosha
mahakama kwa kuwa mambo mengine aliyopinga yako kwenye kumbukumbu za
mahakama.
Kuhusu matumizi ya Sheria za Nchi za Madola, huku
akitoa orodha ya kesai mbalimbali, alidai kuwa kwa mujibu wa kifungu cha
2 (3) cha Sheria ya Uchaguzi kesi za uchaguzi zinaendeshwa kwa mujibu
wa sheria ya uchaguzi na kwamba Jaji alikuwa sahihi kuamua hivyo.
Akizungumzia haki ya mpiga kura kufungua kesi,
Wakili Mughway alidai kuwa haki hiyo inaelezwa katika kifungu cha 111
(1) (A) cha Sheria ya Uchaguzi (2010) pamoja na katiba
No comments:
Post a Comment