Thursday, November 29, 2012

UTAJILI WA MR. BLUE BAADA YA MIAKA KUMI YA KUWA KWENYE GAME YA MUSIC


Staa kutoka ’game’ ya muziki wa kizazi kipya Bongo, Herry Samir ‘Mr Blu’ amesema  nguvu ya zaidi ya 10 aliyoiweka kwenye fani hiyo sasa imemfanya  kumiliki kiasi kikubwa  cha ‘ngawira’ za  kibongo (Shilingi).
Katika Interview ya dakika 45 aliyoifanya na teentz.com, juzi kati, Blu ambaye sasa yuko kwenye  kilele cha Bongo Fleva akisumbua na ngoma yake mpya inayobeba jina la ‘Nipende kama nilivyo’ alifunguka kuwa si mara moja  mtu anaweza  kuzungumza juu ya  kile kinachomhusu kama anachokifanya yeye lakini ameamua kufanya hivyo kwa lengo la  kuwaonyesha watu kuwa kile wanachokifanya wasanii ni kazi ama bishara kama zilivyo  zingine.
“Kwanza, nashukuru kwa kuwa  umenifuata na kuniuliza mambo kama hayo,  ukweli ni kuwa nafahamu ni ngumu kwa mtu kuzungumza  juu ya vitu kama hivyo lakini kwa kuwa tunachokifanya wasanii ni kazi kama zilivyo zingine sina tatizo nitakujibu kila kitu katika  ukweli na kwa ufupi sana” alisema Blu.
Akiendelea Blu ambaye pia  mashabiki wake hupenda kumuita ‘Babylon Baysser’ alisema  kufanikiwa  kwa   wimbo wake wa kwanza ‘Niite Mr Blu’ ndiyo ulikuwa mwanzo wa  mafanikio licha ya  matatizo kadhaa aliyokutana nayo mara baada ya kupata umaarufu.
“Kulikuwana matatizo mengi sana baada ya kufanikiwa kwa ngoma hiyo, lakini nashukuru Mungu kuwa ndani ya muda wote huo  nimefanikiwa kujenga nyumba yangu,kununua gari, na pia akaunti yangu kwa sasa iko poa sana”,
“eee ndiyo natarajia  kuoa, na kwa kuwa tayari nina mtoto haina shaka kuwa mama mtoto wangu ndiye nitakayempa heshima hiyo” kwa hiyo hicho ndiyo ninachoweza kusema kuwa  huo ndiyo utajiri wangu ndani  ya miaka zaidi ya 10 kwenye gemu kwa kuwa nimetumia nguvu zangu kupata vitu hivyo vyote na siku zote Mungu amekuwa akinisimamia” alisema Blu.

No comments:

Post a Comment

sikiliza ngoma zinazo kamata kwa sasa

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...