ALIYEKUWA mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Oliver Mhaiki amesema walijua wazi kuwa Bodi hiyo itavunjwa kwa kuwa ilitoa maamuzi yaliyopingwa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Abdallah Kigoda.
Bodi hiyo ilivunjwa juzi na Dk Kigoda huku akieleza kuwa lengo ni
kuweza kutekeleza nia ya wizara hiyo ya kuboresha utendaji kazi wenye tija na ufanisi katika shirika hilo.
kuweza kutekeleza nia ya wizara hiyo ya kuboresha utendaji kazi wenye tija na ufanisi katika shirika hilo.
Alieleza kuwa Shirika hilo ni nyeti katika taifa,, hivyo ni lazima liimarishwe ili kuhakikisha inafanya kazi kama anavyotarajiwa na wananchi.
Bila kueleza maamuzi iliyoyatoa, Mhaiki aliliambia Mwananchi kuwa Dk Kigoda ameivunja bodi hiyo kwa sababu zake mwenyewe.
Bila kuweka wazi mambo ambayo waliyapendekeza lakini yakapingwa na waziri huyo alisema, “Tulijua lazima ataivunja bodi na ndio maana wajumbe wa bodi hawakushangazwa na maamuzi aliyoyachukua.”

Alipoulizwa sababu za TBS kulalamikiwa na wadau mbalimbali kuwa imeshindwa kutekeleza majukumu yake alisema, “Pale TBS kuna matatizo makubwa mawili, kwanza wafanyakazi ni wachache, hivyo waliopo wanashindwa kufanya kazi ipasavyo kwa kuwa majukumu ya kazi ni mengi kuliko idadi ya wafanyakazi.”
Alisema, “Pia TBS hakuna vitendea kazi vya kutosha jambo linalowafanya wafanyakazi washindwe kufanya kazi kikamirifu, haya matatizo ndio yanayolifanya shirika hili kulalamikiwa kila siku.”
Alisema kuwa mashirika ya Viwango la Kenya na Uganda yameizidi ubora TBS kwa asilimia 75 na kwamba hilo ndio suala ambalo bodi hiyo ilikuwa ikilifanyia kazi, lengo likiwa ni kuirejesha TBS katika ubora unaotakiwa.
Alipoulizwa kuwa kuna habari kuwa moja ya sababu ya kuvunjwa kwa bodi hiyo ni kutoa ripoti ya kumsafisha aliyekuwa Mkurugenzi wa TBS, Charles Ekelege alisema jambo hilo sio la kweli kwa maelezo kuwa uchunguzi kuhusu tuhuma zinazomkabili mkurugenzi huyo bado zinaendelea kufanyika.
“Hilo sio kweli kwa kuwa Ekelege alituhumiw na Kamati ya Bunge ambayo ilitaka ufanyike uchunguzi na CAG akatekeleza agizo hilo na kupeleka ripoti bungeni, sasa hapo tunausika kwa lipi” alisema Mhaiki
Ripoti yenyewe
Mei mwaka huu Bodi hiyo iliwahi kutoa ripoti iliyodaiwa kumsafisha aliyekuwa Mkurugenzi wa shirika hilo, Charles Ekelege.
Ripoti yenyewe
Mei mwaka huu Bodi hiyo iliwahi kutoa ripoti iliyodaiwa kumsafisha aliyekuwa Mkurugenzi wa shirika hilo, Charles Ekelege.
Mapema mwaka huu Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma (POAC) ilitembelea vituo vya ukaguzi wa magari nchini Singapore na mjini Hong Kong, China na kubaini kuwa shirika hilo lina ofisi hewa.
Baada ya kurejea safari hiyo, kamati hiyo ilimlipua Ekelege bungeni ikitaka awajibishwe kwa sababu sio mkweli na kwamba fedha za ukaguzi zimekuwa zikiishia mifukoni mwa wajanja wachache.
Tuhuma hizo zilimfanya Dk Kigoda takribani miezi sita iliyopita kuiagiza bodi hiyo kumsimamisha kazi Ekelege ili kupisha uchunguzi.
Lakini siku chache baada ya Ekelege kusimamishwa kazi baadhi ya wajumbe wa bodi hiyo walitembelea maeneo hayo na kueleza kuwa vituo vya ukaguzi vilikuwepo.
Ujumbe huo wa watu wanne ambao ulijumuisha Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Masharika ya Umma, Mahmoud Mgimwa ilifanya ziara hiyo katika nchi za Japan na China kuanzia Mei 6 hadi Mei 14 mwaka huu.

No comments:
Post a Comment