MZEE wa miaka 75,mkazi wa kijiji cha Mahida anashikiliwa na
polisi wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro kwa tuhuma za kumbaka
mwanafunzi wa darasa la pili mwenye umri wa miaka nane.
Habari zilizothibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa
wa Kilimanjaro jana, Robert Boaz zilisema mzee huyo anashikiliwa katika
Kituo cha Polisi cha Mkuu wilayani Rombo kwa uchunguzi zaidi.
“Yule mtoto amezoea kwenda kuchota maji kwa yule
babu sasa kwa maelezo ya mtoto ni kwamba yule babu alimuingizia kijiti
sio tendo la kubakwa lakini yote hayo ndio tunayachunguza,”alisema Boaz.
Hata hivyo taarifa nyingine zilizowakariri ndugu
na majirani zilidai siku ya tukio hilo Alhamisi iliyopita, mwanafunzi
huyo wa kike alikwenda kuchota maji akisindikizwa na mdogo wake wa
kiume.
“Baada ya hilo tendo watoto walirudi nyumbani na
ndio yule wa kiume akamwambia dada yake hebu mwambie babu (anayeishi
naye) kuwa yule babu amekufanya nini,”alidai mmoja wa majirani.
Jirani huyo ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe,
alidai kuwa yule mtoto alieleza kila kitu na ndipo wazazi walipompeleka
zahanati ya Mahida na baadaye Hospitali teule ya Huruma iliyopo Rombo.
Majirani hao akiwamo Padre mmoja wa Kanisa
Katoliki, walidai baada ya madaktari katika hospitali hiyo ya Huruma
kumfanyia uchunguzi, mtoto huyo alikutwa na Manii sehemu zake za siri.
Kutokana na hasira waliyokuwa nayo majirani hao,
walihakikisha mtuhumiwa huyo anakamatwa na kupelekwa Kituo cha Polisi
Holili lakini baada ya majirani kuchachamaa alihamishiwa kituo cha Mkuu.
No comments:
Post a Comment