MAPADRI wawili wa Kanisa Katoliki Parokia ya Isimani, Jimbo la Iringa, wamejeruhiwa vibaya na kulazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa, kutokana na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi kuwajeruhi kwa silaha za jadi na bunduki, baada ya kuvamia nyumba wanazoishi.
Paroko wa Kanisa hilo Angelo Burgio kutoka Italia
(60) na msaidizi wake Herman Myala walikumbwa na mkasa huo usiku wa
kuamkia jana.
Padri Burgio alijeruhiwa kwa kupigwa risasi mbili
kifuani na kucharangwa mapanga, msaidizi wake Padri Myala alijeruhiwa
kwa mapanga na kuburutwa chini kwenye ardhi.
Tukio hilo limetokea ikiwa ni siku moja tangu
kuvamiwa kwa Kanisa Katoliki Jimbo la Iringa lililopo eneo la Kihesa
mkoani humo, ambapo mlinzi wa kanisa hilo, Batholomea Nzigilwa (65)
alijeruhiwa na kitu chenye ncha kali kichwani.
Nzigilwa amelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa, huku hali yake ikielezwa ikiwa ni mbaya.
Watangaza msamaha
Jana gazeti hili lilishuhudia Padri Burgio akiwa amelazwa, huku akiwa ametundikiwa chupa ya maji wakati akisubiri huduma ya upasuaji kwa ajili ya kutolewa risasi mwilini.
Jana gazeti hili lilishuhudia Padri Burgio akiwa amelazwa, huku akiwa ametundikiwa chupa ya maji wakati akisubiri huduma ya upasuaji kwa ajili ya kutolewa risasi mwilini.
Akizungumza kwa tabu, padri huyo alisema majambazi
hao walifika eneo la Kanisa la Kihesa saa tano usiku wakiwa na silaha
mbalimbali za jadi na bunduki.
Alisema baada ya kumshambulia msaidizi wake, walimfyatulia yeye risasi kifuani wakati alipofungua mlango na kutaka kukimbia.
“Mimi baada ya kuwasikia nilifungua mlango kwa
lengo la kutaka kukimbia ili nijinusuru, lakini hamadi wakanifyatulia
risasi kifuani.
Nilianguka chini na walipoingia ndani walichukua
fedha taslimu Sh3.5 milioni zilizokuwa chumbani kwangu na kisha kunikata
na panga kichwani, ” alisema Burgio.
Hata hivyo, padri huyo alisema, “Sisi
tunawasamehe. Mimi na mwenzangu tumewasamehe tangu walipofanikiwa
kutushambulia na kukimbia. Tunawaombea msamaha kwa Mungu kwani yeye
ndiye anayejua,” alisema Padri Burgio.
No comments:
Post a Comment