Beki wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', Aggery Morris (kulia) akifunga bao la kichwa wakati wa mechi ya kirafiki ya Kimataifa dhidi ya Harambee Stars ya Kenya kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza jan
Time hii nimeitumia kujiunga na bongostaz.blogspot.com kwa ajili ya stori waliyoripoti kwamba timu ya soka ya taifa ya Tanzania Taifa Stars imeifunga Kenya (Harambee Stars) kwa goli 1-0 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza novemba 14 2012 katika mchezo wa kirafiki uliopo pia katika kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).
Hadi mapumziko Stars ilikuwa
mbele kwa bao 1-0 lililofungwa na Aggrey Morris katika dakika ya nne
baada ya kupanda kusaidia mashambulizi ambapo katika mechi hiyo
iliyochezeshwa na refa anayetambuliwa na FIFA Oden Mbaga, Kenya
walitawala dakika 10 za mwanzo, lakini baada ya hapo Stars wakafunguka
nao na kuanza kula nao sahani moja.
Kipindi cha pili Kenya walianza
na mabadiliko huku kocha Henri Michael akiwapumzisha James Situma,
Jerry Santo na Wesley Kemboi na kuwaingiza Christopher Wekesa, Anthony
Akumu na Timbe Ayoub.
Pamoja na mabadiliko hayo mambo
yaliendelea kuwa magumu kwa Harambee Stars kwa sababu wenyeji
waliendelea kucheza kwa makini wakishambulia na kujilinda zaidi huku
kocha wa Stars Mdemnark Kim Poulsen akiwatoa Amir Maftah, Salum
Abubakar, Mwinyi Kazimoto, Mbwana Samatta, Mrisho Ngassa na Thomas
Ulimwengu na kuwaingiza Nassor Masoud ‘Chollo’, Amri Kiemba, Simon
Msuva, John Bocco ‘Adebayor’, Shaaban Nditi na Issa Rashid.
Katika mchezo huo, mshambuliaji wa Kenya anayechezea AJ Auxerre ya Ufaransa alifichwa kabisa na mabeki wa Stars.
Baada ya mchezo huo, kocha wa
Harambee, Mfaransa Michel alionyesha kukerwa na matokeo hayo na kusema
timu yake haikucheza vizuri, wakati Polusen, amefurahia ushindi huo
akisema timu yake haijacheza kwa miezi miwili na baada ya siku mbili za
mazoezi wameifunga Kenya.
Taifa Stars; Juma Kaseja,
Shomari Kapombe, Amir Maftah/Nassor Masoud ‘Chollo’ dk70, Aggrey Morris,
Kevin Yondan, Frank Domayo, Salum Abubakar/Amri Kiemba dk69, Mwinyi
Kazimoto/Simon Msuva dk69, Mbwana Samatta/John Bocco dk 84, Mrisho
Ngassa/Shaaban Nditi dk72 na Thomas Ulimwengu/Issa Rashid dk 89.
Harambee Stars; Frederick
Onyango, Brian Mandela, Eugene Asike, James Situma/Christopher Wekesa dk
46, Edwin Wafula, Jerry Santo/Anthony Akumu dk 46, Peter Opiyo/Charles
Okwemba dk 67, Patrick Obuya, Patrick Osaika/Mulienge Ndeto dk 73,
Dennis Oliech na Wesley Kemboi/Timbe Ayoub dk 46.
No comments:
Post a Comment