TATHIMINI ya mali iliyoharibika kutokana na mvua kubwa iliyonyesha ikiambatana na upepo na kusababisha nyumba kadhaa kuanguka huku nyingine zikiezuliwa paa ni zaidi ya Sh41 milioni.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya mji wa
Njombe, George Mkindo alilimbia gazeti hili ofisni kwake kuwa kazi hiyo
imekamilika na imebaini kuwa mvua hiyo iliharibu nyumba 178.
“Hasara iliyopatikana kutokana na uharibifu wa mvua hiyo ni zaidi ya Sh41 milioni, ambayo imetokana na uharibifu wa nyumba 178, vyakula pamoja na mazao shambani,” alisema Mkindo.
“Hasara iliyopatikana kutokana na uharibifu wa mvua hiyo ni zaidi ya Sh41 milioni, ambayo imetokana na uharibifu wa nyumba 178, vyakula pamoja na mazao shambani,” alisema Mkindo.
Alisema kwa kuwa tathmini imekwishakamilika na
thamani ya uharibifu huo kubainika, hivyo ataituma taarifa hiyo katika
ofisi ya Waziri Mkuu kitengo cha maafa.
Hata hivyo alitoa wito kwa wananchi wa mitaa na
vijiji vilivyokumbwa na maafa hayo kuendelea kusaidiana na waathirika
katika shughuli za ukarabati wa nyumba na mahitaji mengine muhimu,
wakati wakisubiri msaada kutoka Serikalini.
Katika hatua nyingine, waathirika wa mafuriko hayo
wameanza ukarabati wa nyumba zao bila ya kupata msaada wowote kutoka
serikalini.
Uchunguzi wa gazeti hili ulishuhudia baadhi ya
waathirika hao wakikarabati nyumba zao huku wakiitaka Serikali
kuwasaidia kutokana na tukio kutokea bila ya wao kulitegemea na kuharibu
mali nyungi zikiwamo nyumba za mashamba.
No comments:
Post a Comment