Saturday, November 17, 2012

HIZI NDO SENTENSI NNE ALIZOSEMA RAGE KUHUSU KINAONDELEA KWENYE CLABU YA SIMBA IKIWEMO INSU YA GOLIKIPA JUMA KASEJA



ADEN RAGE

Wakati bundi akiendelea kuungura kwenye makao makuu ya klabu bingwa ya kandanda ya Tanzania bara Simba sports club, kutokana na matokeo ya hivi karibuni kwenye ligi ya Premier ya Tanzania bara, leo hii mwenyekiti wa klabu hiyo amezungumza na vyombo vya habari.
Alhaj Ismail Aden Rage, ambae ni mbunge wa Tabora mjini amesema kwamba, anatambua kila kinachoendelea ndani ya klabu, kwa kusema kuwa wapo wanasababisha hali hii itokee hivi sasa, lakini yapo mengi ambayo yamebadilika katika utawala wake.
Hakuishia hapo tu, kwani Aden amesema kwamba kwa niaba ya uongozi wa klabu ya Simba anapenda kuchukuwa fursa hiyo kwa kumuomba radhi nahodha na mlinda mlango wa klabu ya Simba Juma Kaseja, kwa yote yaliyomsibu baada ya mechi dhidi ya Mtibwa Sukari.
Hakuacha kuzungumzia vurugu za vilabu vikubwa vya jiji la Dar es salaam, lakini moja kati ya mambo ambayo uongozi wake umepania kuyafanya, ni kuitoa timu nje ya nchi kwa matayarisho ya duru ya pili ya ligi ya Premier, na mashindano ya kimataifa.
Lakini pia akazungumzia juu ya kusimamishwa uanachama wanachama Ally Bane na Ustadh Masoud, kwa kile alichokiita, kukiuka katiba ya klabu ya Simba.

Pia mwenyekiti huyo amevunja kamati ndogongo zote alizoziteua hapo nyuma, ambazo ni kamati ya mashindano inayoongozwa na Joseph Itang’are Kinesi, ile ya Ufundi iliyokuwa ikiongozwa na Ibrahim Masoud, kamati ya fedha iliyokuwa chini ya Geofrey Nyange Kaburu, kamati ya usajili iliyokuwa chini ya Zakaria Hanspope, na kamati ya nidhamu.

No comments:

Post a Comment

sikiliza ngoma zinazo kamata kwa sasa

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...