KATIBU Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa amesema CCM watazunguka nchi nzima lakini majibu yatajulikana 2015 kwani ndiyo utakuwa mwisho wao.
Pia Dk Slaa amesema Chadema hakiyumbishwi na kuahimia CCM kwa waliokuwa madiwani wake mkoani Arusha, na badala yake kinapata nguvu ya kuweza kusimamia maadili ya viongozi wake.
Dk Slaa alisema hayo jana alipokuwa akizungumza na
gazeti hili kuhusu mambo mbalimbali ya kisiasa yanayoendelea nchini,
ikiwa ni siku moja tangu uongozi wa juu wa CCM ukiongozwa na Katibu Mkuu
wake, Abdulrahaman Kinana umalize ziara yake ya kwanza katika Mikoa ya
Mtwara, Rukwa, Geita na Arusha.
Alisema Chadema siku zote kitabaki kuwa mwalimu na vyama vingine vitafuata kwa kuiga mambo ambayo chama hicho kimeyaanzisha.
“CCM kuzunguka huku na huko na ni kutuiga sisi
kwani tumeanza muda mrefu, baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 tumekuwa
tukizunguka na kuwaeleza wananchi mambo mbalimbali,” alisema Dk Slaa na
kuongeza;
“Wao (CCM) wazunguke tu lakini mambo yote yatajulikana 2015 kwani Watanzania wa sasa siyo wa kudanganywa tena.”
“Wao (CCM) wazunguke tu lakini mambo yote yatajulikana 2015 kwani Watanzania wa sasa siyo wa kudanganywa tena.”
Dk Slaa alisema anashangaa kwa nini CCM
wanazunguka huku wakilalamika wakati wao ndiyo wanaiongoza nchi hivyo
majibu ya matatizo ya wananchi wanayo.“Chadema ni mwalimu na wao
hufuata, waendelee na mzunguko wao lakini waache kulalamika kama sisi
bali watoe majibu kwa kuwa wao ndiyo wanaongoza Serikali,”alisema Dk
Slaa.
Akizungumzia baadhi ya madiwani wa chama hicho
waliohamia CCM, Dk Slaa alisema kuwa hawakiyumbisha chama chao na kwamba
hata kama wamehama wasipolipa Sh15 milioni kama amri ya mahakama
ilivyotolewa watakwenda jela.
Juzi katika mkutano wa CCM Arusha, madiwani wa
Chadema walitangaza kujiunga na CCM huku wakipinga hatua ya Dk Slaa,
kuwa alikuwa akitaka kuwafunga baada ya kuwatimua ndani ya chama hicho.
Madiwani hao ambao walitimuliwa na Chadema
kutokana kitendo chao cha kumtambua Meya wa Jiji la Arusha Gaudensi
Lyimo wa CCM ni Rehema Mohamed, Simba Salum wa Kata ya Kati na Frank
Joseph Takachi wa Kata ya Olasiti.
Jana Dk Slaa alisema kitendo hicho kinaonyesha
jinsi gani kuna wanasiasa ambao ni matapeli hapa nchini kwani madiwani
hao walikwenda mahakamani kutaka warudishiwe uanachama wao sasa
wamekimbilia CCM. “Watanzania sasa wanajua aina ya wanasiasa matapeli,
kama walienda mahakamani kuomba uanachama wanahangaika nini,”alisema Dk
Slaa na kuongeza; “Chama hakitayumba na tutaendelea kusimamia maadili
ndani chama kama ilinavyotakiwa.” Alisema baadhi ya madiwani wameshaanza
kulipa fedha ambazo mahakama imesema, hivyo hao waliokimbilia CCM
wasipolipa fedha hizo ndani ya miezi miwili watakwenda jela kama
mahakama ilivyosema.
NCCR wanena
Katika hatua nyingine Chama cha NCCR-Mageuzi kimemtaka Makamu Mwenyekiti wa CCM, Tanzania Bara, Philip Mangula kushughulikia rushwa ndani ya chama hicho kwa muda wa siku saba na siyo miezi sita kama alivyoahidi.
Katika hatua nyingine Chama cha NCCR-Mageuzi kimemtaka Makamu Mwenyekiti wa CCM, Tanzania Bara, Philip Mangula kushughulikia rushwa ndani ya chama hicho kwa muda wa siku saba na siyo miezi sita kama alivyoahidi.
Kaimu Katibu Mkuu wa chama hicho, Faustin Sungura
amesema vinginevyo chama hicho kitawahamasisha wananchi waikatae CCM
katika Uchaguzi Mkuu wa 2015.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Sungura
alisema wahusika wa rushwa wanafahamika na ametoa siku hizo kutokana na
kuona miezi sita ni mingi na watendaji wa vitendo hivyo wanafahamika
katika chama na Serikali na kwamba kinachokosekana ni dhamira ya dhati
ya kuchagua viongozi wenye mikono safi.
No comments:
Post a Comment