Mwanza
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza,
imemhukumu kwenda jela miezi mitano Katibu wa Chadema Wilaya ya Ilemela,
John Anajus huku ikiwatoza faini ya Sh620,000 viongozi wengine akiwamo
Mkurugenzi wa Oganaizesheni wa Chadema Taifa, Benson Kigaila na madiwani
wawili.
Hukumu hiyo ilitolewa kufuatia watuhumiwa hao
kudharau amri ya mahakama iliyotolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi mkoani
Mwanza, Angelo Rumisha kufuatia kesi namba 69/2012.
Kesi hiyo ilifunguliwa na Henry Matata aliyekuwa
Diwani wa Chadema Kata ya Kitangiri, baada ya kuvuliwa uanachana kwa
kukiuka katiba ya chama, ambaye aliweka pinganizi la kuteua mgombea
umeya Wilaya ya Ilemela.
Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Rumisha alisema mahakama haiwezi kudharauliwa pale inapotoa maagizo yake, hivyo imewatia hatiani kwa kukaidi agizo lake ili iwe fundishi kwao na wengine.
Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Rumisha alisema mahakama haiwezi kudharauliwa pale inapotoa maagizo yake, hivyo imewatia hatiani kwa kukaidi agizo lake ili iwe fundishi kwao na wengine.
Hakimu Rumisha aliwatoza faini ya Sh155,000 kila
mmoja watuhumiwa, huku John Anajus ambaye hakuwapo mahakamani
akihukumiwa kifungo cha miezi mitano jela atakapopatikana.
Watuhumiwa ambao walilipa faini ni Kigaila, Katibu
wa Mwenezi wa Chadema Wilaya ya Ilemela, Kalod Majura, Diwani wa Kata
ya Kirumba, Dan Kahungu na aliyekuwa Meya wa Mwanza ambaye pia ni mjumbe
wa Kamati Tendaji ya chama hicho, Josephat Manyerere.
Katika kesi hiyo, Matata anayetetewa na Wakili
Salum Magongo, aliweka pingamizi mahakamani baada ya Kamati Tendaji ya
Chadema kutangaza kumvua uanachama kinyume cha taratibu na kudai kwamba,
viongozi hao kwa pamoja walishiriki kuvunja sheria kwa kumtangaza
kumfukuza udiwani.
Hivyo, kudaiwa kupuuza amri halali ya mahakama iliyotolewa Septemba 15, mwaka huu.
Hata hivyo, Diwani huyo alivuliwa uanachama na Kamati Kuu ya Chadema Septemba 9, mwaka huu kutokana na madai ya kuvunja katiba ya chama hicho, mpaka kuchaguliwa kuwa Meya wa Manispaa ya Ilemela alikuwa amefungua kesi mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza akiomba mahakama imrejeshee uanachama wake.

Hata hivyo, katika hatua ya kuwanusuru madiwani
hao kufungwa, wananchama wa chama hicho ambao walikuwa wamefurika
mahakamani hapo walichanga Sh250,000 na Sh370,000 zingine zililipwa na
Mbunge wa Ilemela,Samson Kiwia.
No comments:
Post a Comment