Wafanyakazi wa Shirika la Reli
la Tanzania na Zambia (TAZARA)waliopo katika Stesheni ya Dar es Salaam
wamegoma kufanya kazi na kusimamisha huduma zote za usafiri zinazotolewa
na Shirika hilo, wakishinikiza kulipwa mishahara yao.
Wakizungumza na Clouds FM katika ofisi za TAZARA jijini Dar es Salaam kwa sharti la kutotajwa majina yao katika vyombo vya habari kwa kuhofia kuhatarisha ajira zao, wafanyazi hao waliokuwa wamejikusanya katika vikundi vidogo vidogo wamesema kuwa ni mwezi wa pili sasa hawajalipwa mishahara yao.
Wamesema wamekuwa wakiomba malipo hayo kwa muda mrefu bila mafanikio hali iliyosababisha waamue kusitisha huduma mpaka hapo watakapopatiwa ufumbuzi wa kupewa malipo yao.
Wamesema kutolipwa mishahara hiyo ya miezi miwili kumewafanya waishi katika mazingira magumu na familia zao kwani wao ndiyo wanaotegemewa na kuwa kila wanapodai fedha hizo madai yao yamekuwa yakipuuzwa na viongozi kukataa kukutana nao hali iliyosababisha waingie katika mgogoro huo wa kimaslahi na TAZARA.

No comments:
Post a Comment