JUKWAA la Katiba Tanzania limetaka sheria ya mabadiliko ya Katiba irekebishwe ili mchakato wa kupata Katiba Mpya uendelea baada ya Uchaguzi mkuu wa Mwaka 2015 kwa kuwa inahitajika miaka miwili zaidi ya kuweka sheria zitakazosaidia utekelezaji wa Katiba hiyo mpya.
Limesema kuwa ili kuufanya uchaguzi wa Mkuu ujao
kuwa wa haki, bila malalamiko yoyote Ibara ya 98 ya Katiba ya sasa
inatakiwa kufanyiwa marekebisho kwa ajili ya kusuka upya upatikanaji wa
watendaji wa Tume ya uchaguzi ili tume hiyo iwe huru na isifungamane na
upande wowote.
Kauli hiyo imekuja wakati Tume ya Mabadiliko ya
Katiba kesho ikitarajiwa kuendelea na awamu ya mwisho ya ukusanyaji wa
maoni ya wananchi katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Simiyu, Geita,
Mara na Mjini Magharibi.
Akizungumza Dar es Salaam jana Mwenyekiti wa
Jukwaa hiyo, Deus Kibamba alisema ipo haja ya kutenganisha mchakato wa
Katiba Mpya na ule wa uchaguzi mkuu, taifa lijipange kutokuwa na Katiba
hiyo kabla ya uchaguzi ujao.
“Mchakato huu unatakiwa kuendelea baada ya
uchaguzi mkuu na Tume ya Mabadiliko ya Katiba inatakiwa kuongezewa muda
ili ifanye kazi kisheria na sio kukimbiza mchakato huu ili kuwahi muda
uliopangwa na Serikali” alisema Kibamba.
Alitaja hatua zinazohitaji muda zaidi ambazo
zitafuata baada ya tume hiyo kukamilisha hatua ya ukusanyaji maoni ya
wananchi kuwa ni, kuundwa kwa mabaraza ya Katiba, kuandaliwa ripoti ya
ukusanyaji wa maoni, rasimu ya Katiba, Bunge maalumu la Katiba, kupigwa
kwa kura za maoni pamoja na uzinduzi na utekelezaji.
“Haya mambo hayawezi kukamilika 2014, ikumbukwe
kuwa inahitajika miaka miwili baada ya Katiba Mpya kuzinduliwa kwa ajili
ya kufanya maandalizi ya kuweka sheria zitakazosaidia utekelezaji wa
Katiba husika,” alisema Kibamba na kuongeza:
“Maana yake ni kwamba hata tungepata Katiba kabla
ya uchaguzi ujao, hatutakuwa na muda wa kuweza kukamilisha maandalizi
yote ili tuweze kutumia Katiba hiyo mpya kabla ya uchaguzi mkuu 2015.”
Alisema ili kuepusha mvutano katika uchaguzi mkuu
ujao Ibara ya 98 ya Katiba ya sasa inatakiwa kufanyiwa marekebisho ili
ipatikane Tume huru ya uchaguzi.
“Tume hii itakuwa na jukumu la kuandaa wapiga
kura, kusimamia uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka 2014 na Uchaguzi
mkuu wa 2015, pia kusimamia uchaguzi wowote ule utakaofanyika wakati wa
mchakato wa Katiba” alisema Kibamba.
Alisema kuwa unatakiwa kuandaliwa muswada wa
sheria ya mabadiliko ya Katiba utakaoifanya Katiba ya sasa kuzungumzia
uandaaji, usimamizi na uratibu wa uchaguzi wa aina zote kwa mtitiriko
mzuri na kufafanua , “Tunataka tume kuwa na muundo kuanzia ngazi ya
taifa hadi wilaya.”
Alisema kuwa muswada huo unatakiwa kuzingatia
misingi ya uchaguzi mkuu kufanyika sambamba na uchaguzi wa Serikali za
mitaa, maamuzi juu ya uchaguzi kufanyika lini yashirikishe wananchi,
kuzuia vurugu katika uchaguzi,
No comments:
Post a Comment