Mtu mmoja ameuawa na wengine
wawili kujeruhiwa kufuatiaa vurugu zilizotokea leo majira ya saa tano
asubuhi katika eneo la barabara ya Pamba karibu na soko kuu la jijini
Mwanza katika vurugu baina ya wafanyabiashara wadogo maarufu kama
wamachinga na askari wa Halmashauri ya jiji la Mwanza.
Mtu huyo ambaye jina lake kamili halikupatikana badala yake ametambuliwa kwa jina moja tu la Greda.
Taarifa zaidi zinasema kuwa leo
mnamo majira ya saa nne na nusu asubuhi askari wa halmashauri ya jiji
wakiwa katika maeneo yao ya kazi eneo la Pamba road kwenye stendi ya
zamani ya mabasi ya Tanganyika karibu na soko kuu la jiji la Mwanza,
wakiwa katika operesheni zao za kawaida za kusafisha jiji walikamata
bidhaa zilizokuwa zimepangwa katika maeneo ambayo hayaruhusiwi kisheria
wakiwa kwenye eneo hilo mtu mmoja ambaye anadaiwa kuwa ni mmachinga
alimrukia mgambo wa jiji shingoni na kumtolea silaha ya jadi aina ya
sime kwa nia ya kumdhuru.
Baada ya tukio hilo wamachinga
waliokuwa eneo la tukio walianza kuwarushia mgambo hao wa jiji mawe
ndipo wale mgambo wa jiji katika kujihami wakaanza kurusha risasi hewani
kuwatawanya wamachinga hao waliokuwa wakiongezeka kadri kuanza kwa
seleka hilo, kwa bahati mbaya moja kati ya risasi hizo zikampiga mpiga
debe mmoja upande wa kushoto na kufariki papo hapo.
Machinga mwingine amejeruhiwa
kwenye mkono wa kushoto katika kiwiko, naye dereva wa magari ya biashara
za kusafirisha mizigo wa gari aina ya Kenta, magari ambayo hupaki
katika eneo hilo amejeruhiwa upande wa kushoto kichwani na kukimbizwa
hospitali ya rufaa Bugando kwa matibabu.
Mpaka saa tisa alasiri baadhi
ya maduka katikati ya jiji na karibu na eneo la tukio yalikuwa
yamefungwa kabisa licha ya amani kurejea, hiyo ni kutokana na
wafanyabiashara kuhofia usalama.
No comments:
Post a Comment