Mshindi
wa shindano la Epiq Bongo Star Search 2012 (EBSS), Walter Chilambo
(Dar) akikabidhiwa sanduku lake lenye kitita cha shilingi milioni 50
usiku wa kuamkia ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee, katika shindano hilo
lililovuta hisia za wengi, mshindi wa pili ameibuka mwanadada Salma
Abushiri (Zanzibar) na watu ni Wababa Mtuka (Dar).
Mshindi
wa shindano la Epiq Bongo Star Search 2012 (EBSS),Walter Chilambo
(Dar) akiwashukuru wapenzi na msahabiki wake waliompigia kura.
Baadhi
ya mashabiki wa mshindi wa shindano hilo la EBSS,Walter Chilambo
wakishangilia kwa shangwe na vifijo mara baada kutamkwa yeye ndiye
kinara katika kilele cha shindano hilo lililovuta hisia za watu wengi
---
Mshiriki wa Epiq Bongo Star Search
2012 kutoka Dar es Salaam Walter Chilambo usiku wa kuamkia leo amekuwa
mshindi na kujinyakulia kitita cha shilingi za Milioni 50 za Kitanzania.
Walter aliibuka kidedea mbele ya
Salma Yusuf kutoka Zanzibar ambaye walifaikiwa kuingia naye pamoja
fainali ya washiriki wawili tu kati ya watano ambao walianza fainali
hiyo hapo awali. Walter ambaye dalili za ushindi wake zilianza kuonekana
tangu awali mwa fainali hiyo ameweka historia ya kuwa mtanzania wa
kwanza kujinyakulia kitita kikubwa katika mashindano ya kusaka vipaji
vya muziki.
Aidha katika shindano hilo mshiriki
Walter pamoja na wenzake walipitia hatua tatu ambapo ya kwanza ilikuwa
kuimba na msanii mmoja mmoja waliowachagua ambapo yeye aliimba na msanii
Ditto kabla ya kuimba mwenyewe katika raundi mbili zilizofuata huku
wakipigiwa kura na mashabiki katika raundi zote. Walter alitumia nyimbo
moja ya Steve R n B “One Love”, na Nikikupata ya Ben Pol katika raundi
zote mbili zilizofuata.
No comments:
Post a Comment