|  | 
| Brigitte Alfred akipunga mkono kwa furaha mara baada ya kutangazwa kuwa ndie mshindi na kuwabwaga washiriki wenzake 29. | 
 HATIMAYE
 kile kitendawili cha muda mrefu cha Nani ata twaa taji la Redds Miss 
Tanzania 2012, kimeteguliwa usiku wa Novemba 3, 2012, baada ya Mrembo 
kutoka Kitongoji cha Sinza na Kanda ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, 
Brigitte Alfred kutwaa taji hilo.
Brigitte
 ambaye nyota yake katika mashindano hayo ya urembo nchini ilianza 
kung’aa tangu Kitongoji cha Sinza baada ya kutwaa taji la Sinza na Baade
 kutwaa Taji la Redds Miss Kinondoni amedhihirisha ukali wake baada ya 
kuwabwaga warembo wenzake 29 waliokuwa wakiwania taji hilo kutoka Kanda 
mbambali.
Mpinzani
 mkubwa wa Brigitte katika shindano hilo alikuwa ni Mrembo kutoka Kanda 
ya Ziwa ambaye nae alianza kuwika baada ya kutwaa taji la Redds Mkoa wa 
Mara na baade kutwaa taji la Kanda ya Ziwa, Eugene Fabian.
Enagene
 alifanikiwa kushika nafasi ya pili katika shindano hilo kubwa ambalo 
Brigitte ameondoka akiendesha gari aina ya NOAH na kitita cha Shilingi 
Milioni 8.
Nafasi
 ya tatu ilikwende kwa Malkia wa Kitongoji cha Kigamboni City na Miss 
Temeke 2012, Edda Sylvesta huku nafasi ya Nne ikichukuliwa na Mrembo wa 
Dar Indian Ocean na Kinondoni, Magdalena Roy na nafasi ya Tano ikienda 
Kanda ya Ziwa tena kwa Mkoa wa Mwanza, Happyness Daniel.
 
 
No comments:
Post a Comment