Cristiano Ronaldo amesema ana mahusiano
ya kazi tu na mpinzani wake Lionel Messi na sio marafiki na nyota huyo
wa Argentina na Barcelona
Wawili hao wamekuwa wakishindanishwa kwa
kila kitu katika miaka ya hivi karibuni, huku wachezaji wote wawili
wakicheza kwa jitihada kubwa kushinda makombe na tuzo binafsi. Hta hivyo
japo anakiri kwamba hakuna urafiki wa karibu, Ronaldo anasisitiza
hawana ugomvi na Lione Messi na pia akazungumzia heshima yake kwa
mshambuliaji huyo wa Barcelona.
"Yeye [Lionel Messi]ni mchezaji mzuri na
mkubwa sana ," Ronaldo aliiambia beIN sport. "Nina mahusiano ya kikazi
tu na yeye kama niliyonayo na wachezaji wengine. Messi sio rafiki yangu.
kwa sababu hatushei chumba cha kubadilishia nguo. Namheshimu kama
mchezaji. Sisi sio marafiki, japokuwa tuna mahusiano ya kikazi tu.
"Hakuna ugomvi wowote kati yetu japokuwa
kuna baadhi ya watu wanajaribu kutengeneza hali ya namna hiyo, na sio
kitu kipya kimekuwa kikitokea kwa takribani miaka mitano iliyopita.
Siwezi kukizuia."
Ronaldo aliendelea mbele na kusema kwamba anaweza kucheza na Messi timu moja, kitu ambacho hata hivyo amekiri ni kigumu.
"INaweza nikacheza vizuri sana na yeye ikiwa tu atasaini kujiunga na Real Madrid, lakini hilo ni gumu sana," anasema Ronaldo.
TUPE MAONI YAKO
No comments:
Post a Comment