Kuna idadi kubwa ya watu
waliohitaji kufahamu Freemason ni nini baada ya taarifa kuenea kwamba
Freemason ni dini ya kishetani na watu wengi maarufu wamo humo wakiwemo
viongozi wa nchi na mastaa wengine kama Jay Z, Rihanna, Beyonce, Kanye
West, Celine Dion na hata hapa Tanzania june 2012 magazeti ya udaku
yaliwataja wasanii kama Diamond Platnums na Jackline Wolper kwamba wamo
humo lakini wasanii wenyewe walikanusha.
Clouds TV/Radio kupitia kwa
mtangazaji Gerald Hando ilipata nafasi ya kufanya mahojiano na Sir Andy
Chande ambae aliwahi kuwa kiongozi mkuu wa Freemason Afrika Mashariki
kwenye nchi za Tanzania, Uganda, Kenya na Seychelles.
Yafuatayo hapo chini ni maelezo aliyoyatoa.
ALIKOANZIA SIR CHANDE:
Sir Chande: Alifika Tanzania
mwaka 1950, alihamia Dar es salaam 1953 na kukutana na watu wengi wa
bandarini, shirika la reli na mashirika mbalimbali aliyofanyia kazi na
alikutana na watu wengi ambao walikua wanahudhuria vikao vya freemasons,
akaanza kuuliziaulizia na akajifunza mambo kadhaa kuhusu hao watu.
Kwa wakati huo, hao watu
hawakua huru kuzungumzia Freemasons kama anavyofanya chande sasa hivi,
haswa kabla ya vita ya pili ya dunia.
Sir Chande anasema wakati huo
Freemasons ilikua imegawanywa kwenye makundi tofauti, katika
mahospitali, shule, na mashirika mbalimbali na kulikua na kundi maalum
la freemasons kwa ajili ya matajiri na wafanyakazi wakubwa wa serikali,
ukiangalia vizuri wengi wao walikua wazungu na baadhi ya wahindi.
Kundi la kwanza lilikua
linaongozwa na watu wa Scotland, makundi mawili yaliyofata yalikua
yanaongozwa na waingereza na kundi la nne lilikua linaongozwa na wahindi
ambalo kundi la nne ndilo Chande alilojiunga nalo nalo, ilimchukua
miaka miwili kukubaliwa kujiunga na freemason, aliapishwa rasmi rasmi
mwaka 1954 akiwa na umri wa miaka 28, kumbuka kwamba masharti ya
kujiunga na freemasons ni lazima uwe na umri kuanzia miaka 21.
Baada ya hapo ndipo alipoanza
kupenda Freemasons ambapo pia alipanda cheo na kupewa nafasi ya kuongoza
kundi au tawi la freemasons katika nchi nne ambazo ni Kenya, Tanzania,
Uganda na sychels na akajiunga na miradi tofauti ya freemasons nchini
uingereza yakiwemo mahoteli ya kifahari pamoja na kupewa jukumu la
kujenga hoteli mpya ya freemasons nchini Ghana kwenye mji wa Khumasi
ambayo ni ya kifahari sana.
Hoteli nyingine ya kifahari alisimamia ujenzi wake iko Zambia.
Sir Andy Chande kwa sasa ni
mstaafu wa freemasons, 2005 alistaafu kuwa kiongozi wa Freemasons Afrika
Mashariki baada ya kuifanyia kazi kwa miaka 19, kwa sasa haudhurii
mikutano ya hizi nchi za Afrika Mashariki lakini anahudhuria mikutano ya
Uingireza kwa sababu bado anafanya kazi na baadhi ya mashirika
Uingereza.
FREEMASONS NI NINI?
Ni taasisi ambayo ilianzishwa
miaka 350 iliyopita katika njia ambayo haikua rasmi ikaja kuhalalishwa
miaka 300 iliyopita, hatujui vizuri ilianzishwa vipi ila inaaminika
walikua wajenzi wanaojenga mashule, makanisa, wakati ule kulikua hakuna
miji mikubwa kama sasa wala mahoteli, na wao walikua wakiishi pamoja na
familia zao na wakihama wanahama pamoja, wakaanzisha miradi ya kujenga
hoteli ndogo ndogo ili kusaidiana kama wajenzi na kujikwamua kiuchumi,
wakawa wanafundishana.. yani kama una ujuzi unamsaidia na mwenzako kujua.
Anasema “Freemasons
sio dini na tukikuta wewe ni mkristo tunakushinikiza ukristo wako, kama
wewe ni mhindu unabaki kuwa mhindu, lakini freemasons orijino
ilianzishwa na wakristo nchini Uingereza na baadae ikahamia Ulaya,
Marekani, Australia na India Freemasons ikaja kuwa kubwa sana”
NCHI ZA AFRIKA AMBAZO FREEMASON NI KUBWA:
Kwa nchi za Afrika Freemasons
imekuja kuwa kubwa kwenye nchi kama za Nigeria na Ghana pia Sierra
Leone, kwanza aliyewahi kuwa rais wa nchi hiyo Daudi Jawala alikua mmoja
wetu.
Freemasons ilianza mwaka 1646 alafu ikaja kuwa rasmi mwaka 1717 lakini kabla ya hapo katikati ilikua inafanywa kimya kimya.
KAZI ZINAZOFANYWA NA FREEMASON
Kazi zinazofanywa sasa hivi na
Freemasons ni kufundisha wanachama wake kuhusu majukumu yao kwa
mwenyemwezi Mungu, kwa nchi yako, familia, na nchi unayofanyia kazi hata
kama ni ugenini, na kutoa misaada.
WANACHAMA WA FREEMASONS DUNIANI:
Duniani kote sasa hivi kuna
wanachama milioni tatu laki tano wa freemasons na wanachangia dola za
kimarekani zaidi ya milioni 400 kwa ajili ya misaada kila mwaka, yani
kwa siku ni zaidi ya dola milioni moja kusaidia afya, elimu vilevile
wajane wa wanachama wa freemasons wanasaidiwa ambapo pia ukiumwa na
ukiwa na shida yeyote kuna msaada wa bure unapatiwa nakumbuka hata dr
Charles Matwali alipoumwa sana, tulimpeleka uingereza kwa matibabu.
JINSI YA KUJIUNGA NA FREEMASONS:
Ili kujiunga ni lazima uwe na
umri wa miaka 21, ni hiari kujiunga na pia uwe unamwamini Mungu
haijalishi ni Mungu gani, watu ambao hawamuamini Mungu hawaruhusiwi kuwa
Freemasons, na lazima uwe mtu mkweli.
Ni lazima familia yako ikubali
pia wewe kujiunga na freemasons kwa sababu freemasons hawatokubali
kujiunga kwako kukufanye uwe masikini kutokana na kutoa misaada.
Unapotaka kujiunga ni lazima
upeleke maombi yako kwa mtu unaemfahamu ambae yuko Freemasons, au kama
hujui mtu unaandika barua baada ya hapo utapewa nakala za kusoma na
kuelewa na kamati ya kukuruhusu kuingia kwenye freemasons itakupeleleza
wewe na familia yako, na pia watakutembelea nyumbani kuongeana mkeo au
mumeo au familia.
Inaweza kuchukua mwaka mmoja na
nusu au mwaka kuruhusiwa kujiunga na freemasons baada ya kupeleka
maombi, ambapo hapo ni kukubaliwa tu, baada ya hapo ili uwe freemason
kamili kuna vyeo vitatu ambavyo tunaviita degrees ambavyo ni lazima
uvikamilishe jambo ambalo linaweza kuchukua zaidi ya miaka miwili.
BAADA YA KUJIUNGA:
Pia unatakiwa kujifunza vitu
vingi na kuvihifadhi kichwani kama vile maneno ya kusema wakati unafanya
ibada za freemasons kwa sababu tukiwa pamoja tunavyozungumzia sifa za
kuwa binadamu kamili unaweza ukafananisha na ibada ya kanisani.
KUHUSU FREEMASON YA UINGEREZA:
Acha nizungumzie Freemason ya
Uingereza ambayo mimi ni mmoja wao, Makao makuu yako London kwenye
barabara inaitwa great queen street, Mkuu wa Freemasons Uingereza ni
binamu yake malkia Elizabeth ambae tunamuita Grandmaster.
Kazi zote zinazofanyika na
Freemasons zinaendeshwa kutoka kule, kwa mfano mv bukoba ilivyozama
nilipiga simu kule kuomba msaada wakatuma pound elfu 10 ingawa na sisi
hapa tuna kitengo chetu cha misaada ambayo kilichangia, maamuzi ya
misaada mikubwa yanatoka Uingereza.
Kuna mahoteli ya freemasons
Uingereza, Scotland na Ireland na katika nchi zilizokua za kisovieti
zamani, tuna mahoteli duniani nzima ambapo kama upo kwenye freemasons ya
Dar es salaam unaweza kuhudhuria vikao kwenye yeyote kati ya hizo
hoteli duniani tunazomiliki ambazo zinatumika pia kama kumbi za mikutano
yetu ili mradi wawe na uthibitisho kwamba wewe ni mmoja wetu.
Watu wengi huwa wanasema ni
taasisi inayofanya mambo yake kwa siri lakini ukweli ni kwamba siri
pekee iliyopo ni jinsi nitakavyokutambua kama wewe ni mmoja wetu,
vingine vyote viko wazi na vinapatikana hata kwenye internet na unaweza
kwenda kwenye maduka ya vitabu kote afrika mashariki hata uingereza
ukapata nakala zote za freemasons ikiwemo hata maneno tunayosema
tukifanya ibada zetu.
Kwa afrika Mashariki makao
makuu ya freemasons yako Nairobi Kenya kwa sababu aliechukua nafasi
yangu yuko Nairobi na pia makamu wake yuko Nairobi, Kuna majumba 50 ya
freemasons Afrika Mashariki
Ingawa makao makuu yako Nairobi,
jumba la Dar es salaam linajitegemea lenyewe na tunafanya miradi yetu na
kusajili watu wetu hapahapa, hatuingiliwi na ofisi ya Nairobi, maamuzi
yetu yanafanyika hapa hapa.
FREEMASONS WANAPOKUTANA:
Huwa tunakutana saa 12 jioni na
kutoa ripoti ya tulivyovifanya tangu mkutano wa mwisho, kuhusu misaada
tuliyotoa, wanachama wanaoumwa, na nani wa kwenda kumtembelea au kama
kuna mwananchama mpya wa kumuapisha, kama hayupo tunajadiliana kuhusu
mambo tofauti yanayotuhusu isipokua siasa na dini, tunakula pamoja na
kila mtu anaondoka.
MNAKUTANA MARA NGAPI?
Inategemea kama tawi la
Uingereza tulikua tunakutana mara mbili kwa mwaka, la huku ambalo ndiko
nilikoapishwa tulikua tunakutana mara 11 kwa mwaka lakini siku hizi ni
mara kumi, wengine wanakutana mara 5, inategemea na kazi za kufanya,
mfano labda wanachama wa kuapisha ni wengi.
Ibada inafanyikaje?
Ibada inaanza wakati vikao
vinaanza, inahusisha mara nyingi kitu ambacho kinafanana na ibada
kanisani, mara nyingi inahusika kumuweka mwananchama mpya kwenye mstari
na mtazamo mmoja na aliowakuta na kwenye ibada huwezi kuvaa unavyotaka,
lazima uvar suti na tai isipokua nchi kama India ambao hawavai tai.
Ukiwa mwanachama unapewa
maswali ambayo ukiyajibu vizuri kwa muda wako unaweza kupandishwa cheo
na inachukua muda kufikia degree ya tatu, tukiwa kwenye vikao mwenyekiti
anaitwa Master na anao wasaidizi wawili, kwenye ibada mwenyekiti anakaa
mashariki, msaidizi mmoja ana kaa mbele yake akimtizama na wa pili
anakua anasaidia kwa shughuli nzima inayoendelea.
Kuna mwingine ambae ndio
muongozaji wa sala na wakati tukisali, Mungu tunamuita Fundi mkuu
aliyeumba sayari zote hiyo inahakikisha kwamba uwe Musilamu au mkristo
tunakwenda sambamba.
ISHARA ZINAZOTUMIKA FREEMASONS
Kuna alama ya Compass
inayotumika kuonyesha mwelekeo kwa mishale yake, kuna ruler na pembe nne
ambavyo ni vitu vinavyotumika kwenye ujenzi ila vinaweza kutumika
kufundisha kuhusu maisha, na ndio vinatumika hivyo wala sio kuhusu kitu
kingine.
Tukifanya ibada zetu au
kumkubali mtu kuingia freemasons lazima avae pajama au mavazi
yanayotumika kulalia usiku, na haruhusiwi kuwa na pesa mfukoni, kuvaa
saa au cheni ishara ya kuwa yeye ni masikini kama alivyozaliwa.
Uchawi, kuabudu shetani na
mambo kama hayo watu wanayosema kwamba freemasons ndio inajihusisha na
hivyo vitu ikiwemo kutoa uhai ndugu, ni waongo, hawana ujuzi wa kutosha,
nakumbuka pia rais Moi aliunda kamati maalum kuchunguza uchawi na
waabudu shetani na tuliitwa nikaenda kuwaeleza kwa muda wa karibu saa na
nusu kuhusu freemasons, ingawa hawakuja kutupa ripoti kamili
waliyopeleka kwa rais moi, walituambia kwamba wamekubali maelezo yetu na
ingekua bora kama tungekua tunaeleza zaidi watu wajue na tusiwe wasiri.
FAIDA ZA KUWA FREEMASONS:
Hakuna faida za kupata pesa kama
wengi wanavyoambiwa kwamba ukiwa freemasons unapewa mihela, faida za
kuwa freemasons ni pamoja na kuongeza idadi ya marafiki na kuongeza
knowledge (ufahamu)
Faida nyingine labda ni kama
ukitoa tenda kama unaanzisha kiwanda na umetoa tenda ya kazi, ukiona
mmoja wa freemasons yuko kwenye list ya walioomba tenda utampa
kipaumbele kwa sababu unamfahamu na ni kama ndugu.
Hakuna utoaji wa kafara kama inavyosemekana na pia hakuna uhusiano kati ya freemasons na agano la kale.
MAMA MZAZI WA KANUMBA KUHUSU KANUMBA KUWA FREEMASON:
Mama mzazi wa Marehemu
mwigizaji Steven Kanumba alisema siku kadhaa baada ya Kanumba kufariki
kuna kijana alikuja nyumbani na kumwambia mama kwamba yeye (kijana) ndio
alimsaidia Kanumba kujiunga na Freemasons miaka kadhaa iliyopita hivyo
alikwenda nyumbaniili wazungumze na mama, mama Kanumba alimfukuza
hapohapo na kumwambia mwanae hajawahi kuwa freemason na akamwambia
akirudi tena atamwitia polisi.
MISTARI YA JAY Z KWENYE WIMBO WA FREEMASON WA RICK ROSS.
Watu
wananisingizia mambo ya kishetani, uvumi unaenea sehemu zote, nipishe
huyu ni Mungu anafanya mambo yake, najua mnaniogopa Sijui wa kumwamini
sala ya maria inafanya kazi.
Mnanisingizia
vitu vingi vya kishetani lakini bado mnapandisha sauti kubwa
mkisikiliza muziki wangu, hizo stori zote hazina msingi, mniache Mungu
anafanya kazi yake.
Mungu
ndio injinia hapa, asiefanya fanya dhambi atupe jiwe la kwanza
angalieni sura zenu kwenye vioo mnavyoonekana, Sio kwamba mimi ni
Freemason, nilipitia tu mambo mengi sana na Mungu anisamehe manake
nisingefika nilipo bila kufanya dhambi, nimeosha sura yangu kwa maji
matakatifu hii rozari yenye shanga, tena shanga za diamond ni
uthibitisho kwamba Mungu alinisamehe.
Mi ni mkali, acha kutazama kwenye sahani yangu… sema tu unatamani nilichonacho.
No comments:
Post a Comment